Idhaa ya Redio ya UM show

Idhaa ya Redio ya UM

Summary: no show description found

Join Now to Subscribe to this Podcast

Podcasts:

 Watu wa asili wahimiza utunzaji wa misitu, COP20 | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Wakati mkutano wa 20 wa nchi wanachama wa mkutano wa mabadiliko ya tabianchi, COP20 ukiendelea huko Lima, Peru,  jamii za watu wa asili zimetumia jukwaa hilo kupaza sauti juu ya ulinzi wa misitu na utamaduni wa kundi hilo unaotegemea ustawi wa misitu. Basi ungana na Joseph Msami kufahamu kwa kina wanavyotetea rasilimali hiyo.    

 UM waangalia uamuzi wa ICC kuhusu Kenyatta | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

  Umoja wa Mataifa unatathmini uamuzi uliotolewa leo na mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC Fatou Bensouda wa kufuta mashtaka dhidi ya Uhuru Kenyatta.Msemaji wa umoja huo, Stephane Dujarric amesema hayo alipoulizwa na waandishi wa habari tamko la Umoja wa Mataifa kutokana na uamuzi huo wa Ijumaa. (Sauti ya Dujarric) “Bado tunaangalia [...]

 Kampeni ya kurejesha watoto shule yavuna 300,000 CAR, juhudi zaendelea: UNICEF | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Juhudi zinaendelea kuhakikisha maelfu ya watoto wanarejeshwa shuleni katika nchi yenye mgogoro Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR huku hali ya sintofahamu kuhusu usalama wa nchi ikiendelea. Kampeni hiyo inaratibiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ambalo linasema tayari limeshuhudia watoto 300,000 wakirejea shuleni. Watoto ambao wanaorejea shuleni hupatiwa kasha lenye [...]

 Maelfu ya watu wapoteza makazi CAR: UNHCR | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi UNHCR linaonya kuwa zaidi ya watu 850,000 wamepoteza makazi yao nchini Jamhuri ay Afrika ya Kati CAR kufuatia mapigano yanayoendelea. Akiongea mjini Geneva, Msemaji wa UNHCR William Spindler amesema kuwa uwezekano wa idadi hiyo kuongezeka ni mkubwa wakati huu ambapo shirika hilo linahaha kunusuru mgogoro huo uliosababisha hali [...]

 DRC yachukua hatua kuwakomboa watu wenye ulemavu | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Wakati mkutano kuhusu watu wenye ulemavu ukifanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifam, New York, imeelezwa kuwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo DRC  wanawake wanateseka kutokana na mgogoro wa siku nyingi ambao umesababisha ulemavu kwa waume zao. Hali hiyo tete imewalazimu wanawake hao waendelee kukimu  familia zao sambamba na kubeba jukumu la kuwahudumia [...]

 Tujenge mifumo endelevu ya kudhibiti changamoto: Ban | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Baraza la masuala ya kiuchumi na kijamii la Umoja wa Mataifa, ECOSOC leo limekuwa na kikao maalum kuhusu tishio la Ebola kwenye maendeleo endelevu ambapo Katibu Mkuu Ban Ki-moon amesema ni lazima kuweka mifumo thabiti ya afya ya kuweza kukabiliana na changamoto hata za magonjwa. Taarifa zaidi na Amina Hassan. (Taarifa ya Amina) Hadi sasa [...]

 ICC yatupilia mbali mashtaka dhidi ya Kenyatta, Mwakilishi wa Kenya azungumza | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Mwendesha mashtaka wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC huko The Hague, Fatou Bensouda ametupilia mbali mashtaka dhidi ya Uhuru Kenyatta. Taarifa kamili na Grace Kaneiya. (Taarifa ya Grace Kaneiya) Katika taarifa yake Bensouda amesema ushahidi uliopo haujaweza kutosheleza kuthibitisha pasipo shaka madai dhidi ya Kenyatta aliyekuwa anakabiliwa na mashtaka matano ya uhalifu dhidi ya [...]

 Wastani wa bei ya vyakula haikubadilika kwa miezi mitatu mfululizo | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Shirika la chakula duniani FAO limetoa ripoti ya bei ya vyakula kwa mwezi Novemba inayoonyesha kwamba kwa wastani bei ya vyakula haijapanda wala kushuka kwa miezi mitatu  mfululizo tangu mwezi Septemba. Vipimo vya bei vinazingatia mabadiliko ya bei ya vyakula ya kimataifa ikiwemo bei ya nafaka, nyama, bidha zitokanazo na maziwa, mafuta na sukari. Ripoti [...]

 Wanawake DRC wajikwamua kiuchumi | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Uwezeshaji wa wanawake ambao nchi zao zimepitia katika mizozo ni changamoto kubwa ambayo inahitaji kutatuliwa kwa kupitia wanawake wenyewe pamoja na makundi mengine ya kijamii.Nchini Jamhuri ya Kidemokrasi aya Kongo DRC moja ya nchi yenye historia ya mizozo barani Afrika , wanawake wanajitutumua kuchumi kwa kujihusisha katika shughuli zinazowapa fursa hiyo. Langi Asumani wa radio [...]

 Cristina Gallach kuongoza idara ya mawasiliano ya umma ya UM | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemteua Cristina Gallach wa Hispania kuwa msaidizi wake kwa masuala ya habari na mawasiliano kwa umma. Bi. Gallach anachukua nafasi iliyoachwa na Peter Launsky-Tieffenthal wa Austria aliyemaliza muda wake ambapo Ban amemshukuru kwa mchango wake wakati akiongoza idara hiyo. Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imesema [...]

 Ban azungumzia uamuzi wa mahakama New York | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametaka mamlaka zote nchini Marekani kuchukua hatua zipasazo ili kushughulikia madai ya uwajibikaji zaidi miongoni mwa maafisa wanaosimamia sheria. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric  amewaambia waandishi wa habari kuwa wanafahamu kinachoendelea jijini New York, Marekani  kufuatia uamuzi wa Jumatano wa mahakama kutomfungulia mashtaka polisi anayedaiwa [...]

 Maeneo ya urithi wa utamaduni Syria na Iraq yalindwe:UNESCO | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Wakati mzozo ukiendelea huko Iraq na Syrai, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO Irina Bokova ametaka maeneo ya urithi wa utamaduni kwenye nchi hizo yawekewe aina maalum ya kuyalinda. Akifungua mkutano wa kimataifa kuhusu vitisho dhidi ya urithi wa tamaduni na utofauti huko Paris, Ufaransa, Bokova ametaka [...]

 Nyoka waleta kizaazaa huko Sudan Kusini | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Tuanzie Barani Afrika ambako, Watu 13 wamefariki dunia na wengine 10 kuwa katika hali mbaya baada ya kung’atwa  nyoka kwenye Jimbo la Warrap, nchini Sudan Kusini. Ripoti ya Amina Hassan inafafanua zaidi. (Ripoti ya Amina) Kamishna wa eneo hilo Wol Anei Anei amesema uwepo wa nyoka hao unafuatia mafuriko makubwa yaliyosababisha nyoka kukimbilia maeneo makavu [...]

 UNAMID ipatiwe fursa ya kuchunguza tena Tabit:Ladsous | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa hii leo limejadili hali ya usalama na janga la kibinadamu linalogubikwa na kuongezeka kwa uhalifu, ukwepaji wa sheria na raia kukimbia makazi yao katika jimbo la Darfur nchini Sudan. Assumpta Massoi amefuatilia mkutano huo (TAARIFA YA ASSUMPTA) Akihutubia kikao hicho Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za [...]

 Baraza la usalama laani shambulio huko Yemen | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamelaani vikali shambulio la bomu kwenye makazi ya balozi wa Iran nchini Yemen lililosababisha vifo vya watu kadhaa na majeruhi. Katika taarifa yao, wajumbe hao pamoja na kutuma salamu za rambirambi kwa wafiwa wamelaani ktiendo cha kushambulia makazi ya kidiplomasia wakisema kinakwazza kazi za watendaji hao. [...]

Comments

Login or signup comment.