Idhaa ya Redio ya UM show

Idhaa ya Redio ya UM

Summary: no show description found

Join Now to Subscribe to this Podcast

Podcasts:

 Mazungumzo ya Yemen Jumatatu, Ban apongeza | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amekaribisha tangazo lililotolewa na mshauri wake maalum kuhusu Yemen, Jamal Benomar, ya kwamba Jumatatu ataitisha tena mashauriano ya kuleta maridhiano nchini humo. Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imemkariri Ban akipongeza vyama vyote vya siasa na majimbo nchini humo kuwajibika kama viongozi wa nchi hiyo ili [...]

 Shukrani Saudia kwa kujitoa kwa hali na mali: Ban | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Umoja wa Mataifa umeisifu Saudi Arabia kwa jinsi inavyojitoa kwa hali na mali katika kusaidia majanga yanayokumba ukanda huo. Ni kauli ya Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon aliyoitoa wakati alipokutana na waandishi wa habari mjini Riyadhi, baada ya mazungumzo yake na Mfalme Salman bin Abdulaziz wa nchi hiyo. Ban ambaye yuko Saudia [...]

 Nigeria hakikisha kila mwenye haki anapiga kura:Ban | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Kufuatia uamuzi wa Tume ya uchaguzi nchini Nigeria kuahirisha uchaguzi mkuu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amekisihi chombo hicho kuchukua hatua zote za lazima kuhakikisha watu wote wenye haki ya kupiga kura wanafanya hivyo. Ban amesema hayo katika taarifa iliyotolewa na msemaji wake ikieleza kutambua kwake kuahirishwa kwa uchaguzi huo uliokuwa ufanyike [...]

 Hafla yafanyika kuadhimisha wiki ya uwiano baina ya imani mbalimbali | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Hafla maalum imefanyika leo kwenye Umoja wa Mataifa kuadhimisha wiki ya uwiano baina ya imani mbalimbali za kidini. Katika ujumbe wake, Rais wa Baraza Kuu Sam Kutesa, amesema, kutokana na hali ilivyo duniani sasa, ujumbe wa amani na kutenda wema ni muhimu mno, hususan hali ya kutovumiliana na ubaguzi miongoni mwa jamii nyingi. "Wakati kutovumiliana, [...]

 Mbinu endelevu ya wadau mbalimbali unahitajika ili kukuza utali wa kitamaduni | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Mkutano wa utalii wa kitamaduni uliowaleta zaidi ya washiriki 900, ikiwa ni pamoja na zaidi ya mawaziri na makamu wa mawaziri 45 wa Utalii na Utamaduni, wataalamu wa kimataifa, wasemaji kutoka nchi 100, uliondaliwa na  Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO na lile la utalii duniani, UNWTO uliofanyika Siem Reap [...]

 Idadi ya wakimbizi wa ndani Ukraine yakabiria Milioni | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeripoti kuwa mapigano huko Mashariki ya Ukraine kwenye eneo la Donetsk yamesabaisha watu wengi zaidi kukimbia makwao na kwa hivyo kuongeza idadi ya wakimbizi wa ndani kufikia karibu watu milioni moja.Wizara ya Sera ya Jamii ya Ukraine imesema idadi ya wakimbizi wa ndani kote nchini ni [...]

 Wadau wa misaada ya kibinadamu na amani wazuru Sudani Kusini | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu uratibu wa misaada ya kibinadamu Valerie Amos na mjumbe wa amani na upatanishi wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO Forest Whitaker wako ziarani nchini Sudani Kusini ili kutathimini hali ya kibinadamu na kielimu kwa watu walioathiriwa na mgogoro. Wakiwa nchini humo Bi Amos [...]

 Tatizo la chakula lazidi Sudan Kusini:FAO | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Shirika la Chakula na Kilimo FAO limeonya ijumaa hii kuhusu kuzorota kwa hali ya usalama wa chakula nchini Sudan Kusini, huku watu milioni 2.5, sawa na asilimia 20 ya raia wote nchini humo wakiathirika na njaa wakati mapigano yanapoendelea. Mwaka uliopita wakati ghasia ilipoibuka, idadi hiyo ilikuwa ni watu milioni moja tu. Sababu kubwa ya [...]

 Maadhimisho ya kimataifa ya kupinga ukeketaji | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Tarehe Sita mwezi Februari kila mwaka ni siku ya kimataifa ya kupinga ukeketaji wa watoto wa kike na wanawake. Maadhimisho ya mwaka huu yanajikita katika  kukomesha kitendo hicho kinachofanywa siyo tu na mangariba bali pia wahudumu wa afya wakiwamo wauguzi na madaktari. Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, takribani  [...]

 IMF yakwamua ulipaji madeni kwa nchi zilizokumbwa na Ebola | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Shirika la fedha duniani IMF limetoa jumla ya dola Milioni 100 kwa nchi tatu za Afrika Magharibi zilizoathiriwa zaidi na Ebola ili kusaidia ulipaji wa madeni yake. Sean Nolan, Naibu Mkurugenzi wa mkakati na sera IMF amesema nchi hizo ni Guinea, Liberia na Sierra Leone na lengo ni kupunguza athari za mzigo wa ulipaji madeni [...]

 Waigizaji kutoka Uchina wakumbusha historia ya uhusiano wa biashara | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Mwezi huu wa Februari, Uchina ndiyo inayoshikilia kiti cha Urais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Balozi wake Jieyi Liu akiwa na wajibu wa kuongoza vikao vya Baraza hilo. Kama sehemu ya kusherehekea wajibu huo, Ubalozi wa Uchina umeandaa maonyesho ya ngoma na mchezo wa kuigiza, ambao umekumbusha historia ya uhusiano wa kibiashara [...]

 Ebola: Mfumo wa familia Afrika waokoa yatima 16,000 | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Shirika la Kuhudumia Watoto katika Umoja wa Mataifa, UNICEF, limesema kuwa watoto wapatao 16,600 wamesajiliwa kuwa waliopoteza wazazi au walezi wao kutokana na ugonjwa wa Ebola nchini Guinea, Liberia na Sierra Leone.Hata hivyo, UNICEF imesema wengi wa watoto hao wamechukuliwa na jamaa zao, ikisifu ukarimu na uhusiano thabiti wa kijamii. Andrew Brooks ni Mkurugenzi wa [...]

 Mapambano dhidi ya ukeketaji yanahitaji mshikamano: Ban | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-moon amesema inawezekana kukomesha ukeketaji ikiwa jamii nzima itahamasishwa  katika mapambano hayo ambapo kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF zaidi ya wanawake milioni 100 kote duniani huathiriwa. Taarifa kamili na Grace Kaneiya. (TAARIFA GRACE) Katika ujumbe wake kwa njia ya video Ban [...]

 Mdungusi Kakati na manufaa yake kwa afya ya binadamu:FAO | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Mmea uitwao Dungusu kakati, au kwa kiingereza Cactus pear umetajwa na shirika la chakula na kilimo duniani, FAO kuwa zao la asili kwa mwezi huu wa Februari likiwa na manufaa kwa lishe na afya ya binadamu. FAO inasema mmea huo wa jamii ya Mpungate hujulikana kama mkate wa maskini kwenye maeneo ya ukame kwani majani [...]

 Tunaweza kukomesha ukeketaji: Ban | File Type: audio/mpeg | Duration: Unknown

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kupinga ukeketaji, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-Moon amesema inawezekana kukomesha ukeketaji huo unaoathiri zaidi ya wanawake milioni 100 kote duniani ikiwa jamii nzima itahamasishwa kuondokana na kitendo hicho . Katika ujumbe wake kwa njia ya video Ban amesema wataalamu wa afya wana jukumu kubwa katika [...]

Comments

Login or signup comment.